mardi 22 janvier 2013

Viongozi wa Serikali ya Kinshasa watuhumiwa kwa kukwamisha mazungumzo ya Kampala

     
Viongozi wa kundi la M23 wanaoshiriki mazungumzo ya Kampala na Serikali ya DRC
Viongozi wa kundi la M23 wanaoshiriki mazungumzo ya Kampala na Serikali ya DRC
AFP PHOTO/ Isaac Kasamani

Na Emmanuel Richard Makundi
Maofisa wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo DRC mashariki mwa nchi hiyo wamewashutumu waasi wa M23 kwa kuwabadili viongozi wa kijadi pamoja na kuanza kutoza kodi kubwa kwa wananchi.

Waasi hao wa M23 ambao wanashikilia sehemu za mji wa Rutshuru wanadaiwa kuwafuta kazi viongozi wa kijadi kwenye maeneo mbalimbali ya mji huo na kuwaweka viongozi wao ambao wameanza kutoza kodi kubwa kwa wananchi.

Maofisa hao wa Serikali wamesema kuwa wanashangazwa na hatua ya waasi hao kuanza kutekeleza majukumu ambayo hawakukubaliana na Serikali wakati huu ambapo mazungumzo yao yanaendelea mjini Kampala Uganda.

Mbali na viongozi wa mji wa Rytshuru kulalamikia hatua ya waasi wa M23, wananchi pia wameeleza kilio chao na kuonesha kuchukizwa na taratibu ambazo zimetangazwa na waasi hao.

Wakati huohuo viongozi wa waasi wanaoshiriki mazungumzo mjini Kampala Uganda wamekosoa wapatanishi wa Serikali ya Kinshasa kwa kuendelea kuwa kikwazo cha kupatikana suluhu ya mazungumzo yanayoendelea.

Mbunge wa upinzani Roger Lumbala ambaye hivi karibuni alifutwa ubunge wake baada ya kutangaza kuwaunga mkono upande wa waasi, amesema kuwa mazungumzo ya Kampala yanakwamishwa na viongozi wa Serikali ambao wanasimamia mazungumzo hayo.

Kauli ya waasi inapingwa vikali na ujumbe toka Serikali ya Kinshasa ambao umeendelea kusisitiza utayari wao wa kuwasikiliza waasi na kutekeleza yale ya muhimu ambayo yatakuwa na manufaa kwa wananchi wa DRC.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire