samedi 8 décembre 2012

Umoja wa mataifa washtushwa na hali ya usalama nchini DRC

     
Raia wakiwa wamejikusanya kwenye moja ya kifaru kilichotelekezwa na wanajeshi waliokimbia mji wa Goma
Raia wakiwa wamejikusanya kwenye moja ya kifaru kilichotelekezwa na wanajeshi waliokimbia mji wa Goma
RFI

Na Sabina Chrispine Nabigambo
Umoja wa Mataifa umeelezea kushtushwa na hali ya mambo Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mara baada ya kushuhudia maelfu ya raia wakikimbia makazi yao kufuatia kusonga mbele kwa waasi na kuteka miji kadhaa katika taifa hilo,na kutoa wito wa msaada kwa wale walioathirika na ghasia .

Na katika kile kinachotajwa kuwa operesheni kubwa ya kwanza katika shughuli zake za kulinda amani, Umoja wa mataifa umesema kuwa unatazamia kutumia ndege zisizokuwa na marubani kufuatilia mapigano kati ya jeshi na waasi wa M23.
Viongozi wa ukanda wa maziwa makuu wanajielekeza jijini Kampala hii leo kwa ajili ya mkutano kuhusu mgogoro wa karibuni huko Masharaiki mwa DRC eneo lenye utajiri wa madini.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire